Monday, September 13, 2010

Tuchambue Kauli Za Wanasiasa

 WATANZANIA wameaswa kuyachambua kwa umakini yanayozungumzwa katika kampeni za kisiasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ili kung’amua ukweli na uongo.Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, alisema hayo wiki hii mjini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).Alisema katika kipindi hiki cha kampeni yatazungumzwa mengi, ikiwa ni pamoja na ahadi zisizotekelezeka kama za utoaji wa elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu na kufuta kodi.“Tuwasikilize, tupembue chuya zikae upande wake, chenga upande wake na mchele ukae upande wake, tuseme lilo la kweli, kama serikali haitatoza kodi, itaendeshaje shughuli zake?” Alihoji na kujibiwa “hatudanganyiki mama”. Mama Salma ambaye kitaaluma ni mwalimu, alisema gharama zinazotozwa na serikali kwa wazazi na walezi katika elimu, ni ndogo sana ikilinganishwa na za nchi nyingine.Akizungumzia baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu, Mama Salma kwa kiwango kikubwa yameboreshwa ikilinganishwa na wakati wake alipokuwa akifundisha.Alisema kwa miaka zaidi ya miaka 15 ambayo amefanya kazi ya ualimu, maslahi ya walimu yalikuwa duni, lakini katika kipindi cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya nne yameboreshwa ikiwa ni pamoja na walimu kupandishwa na madaraja na mishahara kuongezeka.‘’Nimefundisha kwa miaka 16 mshahara wangu ulikuwa hauzidi sh. 150,000, lakini kwa sasa hali siyo hiyo, yamefanyika maboresho makubwa katika masilahi ya walimu,” alisema.Mama Salma alisema kuongezeka kwa shule za sekondari nchini, ni uthibitisho kwamba serikali ina dhamira ya dhati ya kuwaletea wanachi maendeleo kwa sababu nchi zilizoendelea zimewekeza katika elimu ya watoto na vijana wao.Aliwasisitizia wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kutokuona aibu ya kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya 2005.

No comments:

Post a Comment